Saturday, August 24, 2013

WAFANYE WATABASAMU WATEMBELEA TENA WATOTO MUHIMBILI LEO

Mchoraji katuni wa magazeti ya Mwananchi, ambaye pia ni mdau wa mradi wa Wafanye Watabasamu, Masoud Junior, akichora na baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, leo. Mradi huo ulioanzishwa na kuratibiwa na Nathan Mpangala, hutembelea watoto waliolazwa kipindi kirefu mahospitali ili kuwafariji, kuwapa zawadi kisha kuchora nao michoro mbalimbali. Uchoraji kwa watoto wagonjwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia kama inavyoonekana katika picha, kwani pamoja na maumivu waliyonayo, waliweza kunyanyuka vitandani na kujiachia sakafuni

Mkurugenzi kitengo cha mawasiliano SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, akiteta jambo na wachoraji nje ya Jengo la Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, leo, walipokutanishwa na mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Nathan Mpangala. Mradi huo hutembelea watoto waliolazwa hospitalini muda mrefu, ukilenga kuwafariji, kuwazawadia zawadi, kisha kuchora nao michoro mbalimbali ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. Kutoka kushoto ni Gadi Ramadhani (Art Director), Nathan Mpangala (ITV, mwanzilishi/mratibu wa mradi), Said Michael (Tanzania Daima), na Abdul King O (Nipashe)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...