Monday, August 19, 2013

ZAIDI YA TANI 21,000 YA SHEHENA YA MAHINDI YANUNULIWA NA WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA MKOANI RUVUMA

 Mkuu wa mkoa wa ruvuma aliyenyoosha mkono akiangalia shehena ya mahindi yaliyonunuliwa na wakala wa hifadhi ya taifa ya chakula mkoani ruvuma ambapo hadi sasa zaidi ya tani 21,000 zimeshanunuliwa kwa muda wa wiki mbili tu ikilinganishwa na idadi ya mwaka uliopita ambao tani 27,000 ndizo zilizonunuliwa
Mwambungu kulia, akizungumza na waandishi wa habari mjini songea hawapo pichani kuhusu kazi ya unuzi wa mahindi unavyoendelea katika mkoa huo,katikati ni meneja wa wakala wa hifadhi ya taifa ya chakula morgan mwaipyana na kushoto meya wa manispaa ya songea charles mhagama

 ----------------------------------------------------
Na Cresensia Kapinga wa Demashonews, Songea.

WAKALA wa hifadhi ya chakula ya Taifa mkoani Ruvuma (NFRA) wanatarajia kununua tani 50,000 za mahindi katika msimu wa mavuno wa mwaka huu na tayari  wameshanunua tani 21,000 za mahindi ndani ya wiki tatu tangu msimu ulipofunguliwa.

Akizungumza ofisini kwake jana na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mambungu alisema kuwa mwaka huu  wakulima wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuuza mahindi yao kwenye hifadhi  ya chakula kutokana na bei iliyopangwa na serikali kuwa nzuri tofauti na za walanguzi.

Alisema kuwa  lengo la serikali kununua tani elfu 50 za mahindi na kwamba mwaka huu kasi ya ununuzi imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo lengo lilikuwa kununua tani elfu 50 walinunua tani elfu 26 tu  ambazo tayari zimeuzwa ndani ya nchi na zingine zimeuzwa nje ya nchi.
Alisema kuwa tayari wameshapata fedha za ununuzi wa mahindi kwa awamu ya kwanza ambazo zimeisha na majuzi tayari wameletewa tena kiasi cha sh.bilioni 3 na kwamba wananunua kwa kilo moja ya mahindi sh.500 kiwango ambacho ni halali na  kitawasaidia wakulima kuinua kipato chao.
Hata hivyo amewataka wakulima kuyahuza mahindi yao kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa kwani wanahifadhi mahindi kitaalam na kwa sababu ni hifadhi ya taifa itawasaidia pindi watakapoishiwa chakula watauziwa kwa bei ya nafuu  tofauti na wafanyabiashara wengine.

''Tumewapiga bao wafanyabiashara ambao kazi yao ni kuwalalia wakulima kwa kununua mahindi bei ya chini lakini hata hivyo serikali haimzuii mfanyabiashara yeyote yule kununua mahindi kwa wakulima isipokuwa wafuate bei ya alali iliyopangwa na serikali na atakaye nunua mahindi kwa bei ya chini ya sh.500 akibainika atachukuliwa hatua za kisheria."alisema Mwambungu.
Mwambungu  ameonya vitendo vya baadhi ya wakulima kutokuwa waaminifu pindi wanapopeleka mazao yao kwenda kuyauza mala nyingi wanachanganya na takataka kitendo ambacho amesema si cha kiungwana hata kidogo.

Hata hivyo ametoa rai kwa wakulima kutumia vizuri mapato wanayopata ili yaweze kusaidia kuinua kiwango cha maisha ya familia ikiwemo kusomesha watoto na baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuchukuwa mapato na kufanyia mambo nje ya familia zao ni vyema wakajiepusha kwa kuzibadilisha familia zao.

Aidha watu zaidi ya 500 tayari  wamepata ajira mbalimbali kwenye hifadhi hiyo ya chakula ikiwemo ya kuchekecha mahindi na zingine ambazo zitasaidia kuinua viwango vya maisha yao ya kila siku tofauti na walipokuwa hawana kazi.
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...