Friday, September 13, 2013

BINTI AKUTWA AMEKUFA KATIKA CHUMBA CHA KUFANYIA BIASHARA DAR

WANANCHI KATIKA ENEO LA TUKIO

BAADHI YA MAJIRANI KATIKA ENEO LA MWANANYAMALA KISIWANI WAKIKUSANYIKA KUSHUHUDIA MWILI WA BINTI HUYO

MAMA MWENYE NYUMBA AKIMPATIA MAELEZO MTANGAZAJI WA RADIO ONE STEREO OMARY KATANGA ANAETAZAMANA NAE KULIA JINSI TUKIO LILIVYOTOKEA

MWILI WA ASHA RASHID HUSSEIN ALIYEFARIKI KATIKA CHUMBA CHA BIASHARA WAKATI AKITENGENEZA CHAPATI KUSHOTO KWAKE INAONEKANA CHAPATI ALOKUWA ANAITENGENEZA

WANAHABARI WAKICHUKUA PICHA MBALI MBALI ZA MWILI WA MAREHEM KATIKA ENEO LA TUKIO
Msichana mmoja aliyetambulika kwa jina la Asha Rashid Hussein amekutwa amekufa katika chumba ambacho huwa anafanya biashara ya vyakula katika eneo la mwananyamala Kisiwani karibu kabisa na bar ya Paradise.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne wakati binti huyo alipowasha moto katika chumba hicho Alfajiri kwa ajili ya kutengeneza chapati kwa ajili ya chai kwa wateja wake ambao kwa kawaida huwa wanakwenda kununua chai mahali hapo kila siku asubuhi.

Akisimulia jinsi alivyogundua tatizo hilo mama mwenye nyumba ambako tukio hilo limetokea,amesema alishangaa kuona hadi asubuhi ile mlango wa sehemu hiyo ya biashara ulikuwa haujafunguliwa na haikuwa kawaida kwa Asha kwani huwa anafungua mapema sana.

Alipojaribu kuusukuma akagundua kuwa mlango  huo ulikuwa umerudishwa tu na kuwekwa komeo dogo kwa ndani,walipochungulia ndipo akamuona bvinti huyo kalala huku chapati alokuwa anatengeneza ikiwa kwenye kibao na jikoni alikuwa kabandika chai.

Baadae polisi walipofika eneo la tukio walifungua mlango huo na kuuchukua nmwili huo hadi katika hospitali ya Mwananyamala.

Diwani wa kata hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kupata ripoti ya daktari,amesema sababu ya kifo cha binti huyo ni kuvuta hewa ya sumu inayotoka kwenye mkaa kabla haijakolea Carbon Monoxide ambayo kwa kawaida kama ukiwasha mkaa na eneo husika likawa halina sehemu ya kutosha kupitisha hewa basi husababisha umauti kwa dakika chache sana.

Katika chumbga alichokutwa Asha amekufa hakukuwa na dirisha hata moja na alijifungia wakati anawasha moto huo.

Binti huyo alizikwa juzi kijijini kwao huko kibaha mkoani pwani na habari zinasema alikuwa mgeni katika eneo hilo na ndiyo kwanza alikuwa ameletwa kwa ajili ya kufanya kazi ya mama lishe.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Asha Rashid Hussein mahala pema peponi Amin.

1 comment:

  1. ooh what a sad story jamani.... RIP Asha Rashid Hussein

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...