Tuesday, September 3, 2013

MWANAMKE ALAZWA HOSPITALI AKIJARIBU KUTOA TUMBONI FEDHA DOLA 5,000 ZA MAREKANI ALIZOZIMEZA

Christie Black
Mwanamke wa kimarekani Christie Black(43),amelazwa hiospitalini baada ya kuumia vibaya kooni na tumbaoni wakati akijaribu  kutoa kiasi kikubwa cha fedha alizozimeza kwa kutumia ufagio wa kusafishie choo.

Christie mkazi wa Bulls Gap katika jimbo la tennessee alipata majuraja hayo baada ya kushindwa kutoa dola za kimarekani 5,000, sawa na shilingi milioni nane za Tanzania alizomuibia mpenzi wake Bobby Gulley.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi wa jimbo hilo,Christie alichukua uamuzi huo ili kukwepa kugawana fedha hizo na mpenzi wake huyo baada ya kutengana.

Taarifa zinasema mara baada ya kujiingiza ufagio huo kupitia mdomoni,mwanamke huyo alisikia maumivu makali kutokana na michubuko iliyosababisha atokwe na damu nyingi sana mfululizo.

Inasemekana hali yake inaendelea vizuri hospitalini hapo baada ya kuwwahishwa na kupatiwa matibabu kwa haraka.

Ppolisi wanasema walipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa mpenzi wa Christie,Bobby Gulley ambae alikwenda kushitaki kuibiwa fedha hizo na baada ya upelelezi walimbaini mwanamke huyo ndiye muhusika wakati yuko taabani hospitali.

Christie alipoulizwa kuhusu sababu ya kumeza kiasi hicho kikubwa cha fedha,alisema alikuwa anataka zikamsaidie kimaisha baada ya kupata taarifa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa na mpango wa kumuacha.

Mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya wizi wa fedha na mara atakapopata nafuu atapandishwa kwa pilato ili kujibu mashitaka yake hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...