Hali
ya amani Imerejea jijini Mbeya muda huu baada ya Jeshi la Polisi
Kudhibiti Vurugu hizo ambazo wafanya Biashara waliandamana kupinga Bei
za Mashine za TRA, Utulivu huo umetokea baada ya Jeshi la Polisi
Kutangaza kuwa kila mtu arejee kwao na kuwasihi wananchi wasifanye tena
fujo hizo.
Magari ya Jeshi la Polisi yakiwa yanazunguka kila upande kuhakikisha kuna usalama wa kutosha
Sasa safari za Daladala Mwanjelwa zinaendelea kama kawaida
Ulinzi mkali umeimarishwa pembezoni mwa Maduka ili kuepusha uharibifu wa vibaka ambao wanaweza vamia maeneo hayo
Huu
ni moja ya mitaa ambayo imechangamka sana kwa Mfikemo lakini leo hali
imekuwa kimya hakuna hata sehemu moja iliyo wazi kote kumefungwa .
Hii ni Mitaa Mbalimbali ya Mwanjelwa ambapo Maduka yote yamefungwa hakuna aliye fungua siku nzima ya leo ..
Gari
la kumwaga maji ya kuwasha kutoka Jeshi la Polisi Likiwa limesimama
tayari kwa lolote ambalo litatokea muda huu na mpaka baadae...
Mpaka
sasa hivi tunapo toa ripoti hizi za moja kwa moja kutoka Jijini Mbeya
kutokana na vurugu kubwa iliyozuka kwa wafanya biashara kugomea mashine
za TRA, Sasa wafanya biashara hao wamerejea makwao ingawa kulikuwa na
vugu vugu la Vijana vibaka kuleta vurugu lakini nao Jeshi la polisi
limeweza kuwadhibiti wote na hali sasa imekuwa tulivu... Ingawa kulikuwa
na Minong'ono kutoka kwa watu mbalimbali wakiomba hali hii kesho iwe
shwari na kusiwe na vurugu tena...
Tone
multimedia Live group kupitia Mtandao wetu wa Mbeya yetu ndio tulikuwa
tunawaletea tukio zima kuanzia Mwanzo mpaka sasa tunaondoka eneo la
tukio...
No comments:
Post a Comment