Wednesday, October 2, 2013

WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WALIOKOSA MKOPO WAFIKISHA MALALAMIKO YAO WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI LEO


BAADHI YA WANAFUNZI WA VYUO MBALI MBALI VYA ELIMU YA JUU WAKIWA NJE YA JENGO LA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

LANGO LA WIZARA

BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA NJE YA JENGO

WAKIINGIA WIZARANI

WAKISIKILIZIA NJE YA GATE

WAKIWA NJIANI KUELEKEA

KATIKA MISURURU KUELEKEA WIZARANI


Wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu hapa nchini leo wameenda kwa misusuru hadi wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ili kujua hatma ya mikopo yao.
Wengi wa wanafunzi hao wameonesha kukerwa na hali hiyo kwa sababu wanashindwa kufanya mambo yao ya msingi katika taaluma zao kwa kuwa hali kwa sasa si nzuri kwao na  inaweza kusababisha wakashindwa kuzingatia zaidi kilichowapeleka chuoni kutokana na ukosefu wa fedha za kujikimu.

Baada ya kufika wizarani hapo walipokelewa na kupewa agizo kuwa wachague wawakilishi wao kwani hawawezi woote kuingia  ndani kuwasilisha madai na malalamiko yao.

Kumekuwa na tatizo karibu kila mwaka wa masomo unavyoanza hasa kwa baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kukosa mikopo kutokana na sababu mbali mbali.

Blog hii hadi inaondoka eneo la tukio hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu hatma ya wanafunzi hao kupata mikopo yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...