Sunday, October 20, 2013

TANZIA;MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGAH AMEFARIKI DUNIA MKOANI MOROGORO ASUBUHI HII

Mtangazaji mahiri mwenye sauti tamu ya kuvutia Julius Omang'era Nyaisangah amefariki dunia mkoani Morogoro leo asubuhi.Nyaisanga amefariki katika hospitali ya mazimbu inayomilikiwa na chuo kikuu cha Kilimo SUA,na mwili wake umehamishiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhifadhiwa.Taarifa za awali zinasema Julius Nyaisanga alizidiwa jana akiwa nyumbani kwake Kihonda Mkoani humo na kukimbizwa katika hospitali hiyo ya mazimbu kabla mauti hayajamkuta leo asubuhi.

Nyaisangah anakumbukwa kwa umahiri wake katika kufanya vipindi mbalimbali hasa sauti yake ambayo ilikuwa na mvuto wa kipekee na alianza kuvuma wakati yupo Radio Tanzania Dar es Salaam hasa kwenye vipindi vya club raha leo show,misakato na disco show na taarifa za habari kabla hajahamia ITV/Radio One akiwa ni mmoja kati ya waanzilishi wa vituo hivi ambapo aliwika katika vipindi vya sunday special,hizi nazo,habari nyepesi,nyepesi,mambo mseto na taarifa za habari kabla ya kuondoka na kuhamia Abood media group.Julius Nyaisanga alijulikana pia kwa jina la uncle J,super tall na babu wa kimanzichana ameacha mjane na watoto watatu.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Ameen,angalia baadhi ya picha akiwa katika matukio mbali mbali.
MDAU AKIMUONESHEA KIDOLE JULIUS NYAISANGA
AKIPATA CHAKULA WAKTI ALIPOKWENDA JAPAN
AKIWA KATIKA SHOPPING MALL JAPAN
JULIUS NYAISANGAH
AKIWA NA ABUBAKAR LIONGO NA MDAU MKOANI MOROGORO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...