Tuesday, November 12, 2013

AKOSA KAZI KUTOKANA NA KUWA NA VIDOLE 12 SASA ATAKA KUHAMIA UINGEREZA

Man with 12 fingers seeking typist job
VIJAY SINGH AKIONESHA MIKONO YAKE YENYE VIDOLE 12
Vijay Singh mzaliwa wa India aliezaliwa na vidole 12 anataka kuhama India kwenda Uingereza kutafuta kazi ya ukatibu muktasi baada ya kutafuta kazi nchini mwake bila mafanikio licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuchapa maneno 100 kwa dakika.

Vijay ambae pia anavidole 12 vya miguu sita kila upande anampango wa kuhamia Uingereza baada ya kushindwa kupata kazi India ya kutuma maombi ya kutafuta kazi 50.

Vijay mwenye umri wa miaka 48 kutoka Agra kaskazini mwa India anasema sehemu nyingi alizoomba kazi wanataka msichana mrembo na si mwanaume tena mwenye vidole 12.

Tofauti na watu wengine ambao huwa na vidole vya ziada lakini havifanyi kazi,kwa Vijay ni bahati kubwa kwani vidole vyake vyote 12 vinauwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa speed ya hatari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...