SAFARI YA KUELEKEA DSM YAANZA
MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA
SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA JIJI
NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE WAWILI
AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO,
MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA
MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM.
BAADA YA UTAMBUZI NDUGU
HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA ALIKUWA ANAITWA
KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO,
MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.
AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA
MBEYA. KASSIM SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA AKIWA KATIKA
TARATIBU ZA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI
KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA
LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI
DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA
RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA
KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO
SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.
BASI HILO BAADA YA
KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA
ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI,
MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA GARI
HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI
KUDHOOFIKA.
WAHUSIKA WA GARI WALITOA
TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI
YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA
HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
MWILI WA MAREHEMU
ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA
ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI
YA PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA, PIPI HIZO ZINA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140.TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI
WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA MADAWA HAYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU
KAZI YA TAIFA.
Signed by:
[DIWANI
ATHUMANI- ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment