Watoto watatu wa familia moja ambao walikuwa wamepanda pikipiki wamekufa baada ya kugongwa na basi la Mtei express katika njia kuu itokayo Singida hadi Arusha ambapo baada ya tukio hilo wananchi wenye hasira waliamua kulichoma moto basi hilo.
Kamanda wa polisi mkoani Singida SACP Gefrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Mtei Express lenye usajili wa namba T 742 ACU lilikuwa likitokea Singida na kuelekea jijini Arushana pikipiki aina ya Slag yenye usajili wa namba T368 BXZ ambayo ilikuwa imepakia watoto watatu na baba yayo akiendesha.
Katika hatua nyingine kamanda Kamwella amewataja waliokufa papo hapo ni Tabiri Shabani,Kasimu Shabani na Hamza Shabani kafa wakati akipatiwa matibabu na dereva wa pikipiki ambaye ni baba wa watoto hao amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo ambaye naye alikuwa abiria bwana Nakomolwa Thomas amesema dereva wa pikipiki aliamua kukata kona upande wa kulia bila ya kuangalia kama nyuma kuna basi lina kuja na kusababisha kugongwa na basi na kuburuzwa hadi pembeni mwa barabara.
Naye Nganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktali Banuba Deogratius amesema wamepokea maiti mbili , mtoto moja amefariki wakati wanampatia huduma na mwingine ambaye ni baba watoto hao bado anaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment