Friday, January 10, 2014

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO MKOANI TABORA


Watu wawili wamekanyagwa na tembo na kupoteza maisha katika kitongoji cha Nyampindi wilayani Uyui mkoani Tabora ,  huku familia tisa zikikabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na akiba yao kuliwa na wanyama hao, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wananchi wanalima na kuishi katika njia za tembo hao.

Hayo yamebainishwa na mtendaji wa kijiji cha Songambele kata ya miyenze wilayani Uyui mkoani Tabora Bi Malieta Makenga wakati akitoa taarifa kwa mwenyekiti wa umoja wa wabunge wanaojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyamapoli, tembo na faru pamoja na vyanzo vya maji waliokwekuwa katika kukagua hali ya uhalibifu wa mazingira, katika mikoa ya Lindi, Rukwa Katavi na Tabora.

Akizungumza na wananchi waliokumbwa na adha hiyo katika kijiji cha Songambele, mwenyekiti wa umoja huo Mhe. Riziki Saidi Ruliga, mbunge viti maalum CCM mkoa wa Lindi, amesema kuwa pamoja na kuwepo uharibifu mkubwa wa mazingira, ameitaka serikali kuanzisha rasmi tume ya haki za wanyama, kwa lengo la kuhifadhi wanyama hao.

Aidha akizungumzia fursa za wananchi katika kupambana na mauaji ya wanyama ambao ni rasilimali za taifa, makamu mwenyekiti wa umoja huo mbunge wa jimbo la Igarula Mhe. Mhandisi Dk Athumani Mfutakamba amewataka wananchi kwa pamoja kuwa na mshikamano wa kuchukia vitendo vya ujangili, vinavyofanywa na baadhi ya watu na kutoa taarifa za siri ili watiwe mbaloni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...