Tuesday, January 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA SARAFU YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI IKULU DAR LEO.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo  kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (kushoto) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu baada ya kukabidhiwa Sarafu maalum ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito wa g 16, baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiitazama  Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, baada ya kuipokea kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka  hayuko kwenye picha wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo  kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...