Saturday, February 22, 2014

WAJUE MABILLIONEA WA DUNIA


HAWA NDIYO MABILIONEA WA DUNIA

Viwango vipya vimetolewa vinavyoonyesha watu matajiri zaidi duniani,kwa mujibu wa mtandao wa forbes kwa mwaka 2013 idadi imeongezeka hadi kufikia majina 1,426,na utajiri wao unafikia hadi dola za kimarekani trillioi 5.4 kutoka dola trillion 4.6.

Majina mapya yaliyoongezeka ni 210 na kwa mara nyingine matajiri wa Marekani wameendelea kuongoza kwa kuwa na mabilionea 442,wakifuatiwa na Asia 386, Europe 366, Mashariki ya kati na Africa 103.

 Carlos Slim kwa mara nyingine ameongoza kuwa billionea namba moja duniani akifuatiwa na Bill Gates. Amancio Ortega wa Hispania amekuwa wa tatu kwa mara ya kwanza.

Amekuwa mtu ambae ameingiza pesa kwa kiasi kikubwa kiasi cha dola billioni 19.5 kwa mwaka mmoja ambapo amempita Warren Buffett ingawa mwekezaji huyo wa kimarekani ameongeza dola biloni 9.5, huu ni mwaka wake wa kwanza kuwa nje ya tatu bora tangu mwaka 2000.

Mtu ambae ametia fora kwa kushindwa kuliko wote ni mbrazil Eike Batista ambae amedondoka kutoka kujiingizia kwa mwaka dola bilioni 19.4 sawa na dola millioni 50 kwa siku na amedondoka hadi nafasi ya saba kati ya matajiri 100 duniani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...