Waanzilishi wa Whatsapp: Brian Acton na Jan Koum.
Katikati ya mwaka 2009, Brian Acton alikuwa software engineer ambaye
hakuna kampuni iliyotaka kumwajiri. Pamoja na uzoefu wa miaka zaidi ya
10 kama mwajiriwa wa Yahoo na Apple Computer, alitosa kuajiriwa kwenye
makampuni ya Facebook na Twitter.
Kwanza walikuwa Twitter waliomkataa mwezi May. Tarehe 23, May mwaka
2009, Brian Acton alitweet: Got denied by Twitter HQ. That’s ok. Would
have been a long commute.”
Kisha Facebook waliokataa kumchukua mwezi August. Tarehe 3 August,
2009 akatweet: Facebook turned me down. It was a great opportunity to
connect with some fantastic people. Looking forward to life’s next
adventure.”
Baada ya Acton kukosa kazi kwenye makampuni hayo, aliamua kuanzisha
kitu chake mwenyewe. Aliamua kuungana na aliyekuwa mwajiriwa mwenzake wa
Yahoo, Jan Koum, kuanzisha WhatsApp, ambayo leo imekuwa mfalme wa
mawasialino ya ujumbe duniani. WhatsApp inatawala vichwa vya habari wiki
hii sababu Facebook imekubali kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni
19.
Akiwa na asilimia 20 ya hisa kwenye kampuni, Acton atakuwa tajiri wa
dola bilioni 3. Historia yake imegeuka kuwa funzo la watu kutokata tamaa
kwa wale wanaotafuta kazi. Story yake pia itawapa uchungu waajiri.
Kuajiri watu sahihi ni jambo la bahati lakini hakuna kampuni kubwa
duniani itapenda kuwa maarufu kwa kuacha Brian Acton mwingine aondoke.
Chanzo: Forbes/Kamanda wa matukio
No comments:
Post a Comment