WAHABESHI WALIOKAMATWA NA UHAMIAJI MKOANI TANGA |
MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO |
WATANZANIA WALIOKAMATWA WAKIWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU KUSHOTO NI ALHAJ MIRAJ SHIMBO NA KULIA NI HALFAN MWAVESO |
OFISI YA UHAMIAJI MKOA WA TANGA |
ALHAJ MIRAJI SHIMBO MMOJA WA WATUHUMIWA |
HALFAN MWAVESO MTUHUMIWA WA USAFIRISHAJI WAHAMIAJI HARAMU AKIANGUA KILIO WAKTI AKITOA MAELEZO |
AFISA UHAMIAJI WA MKOA WA TANGA BW SIXTUS NYAKI |
KILIO KIKIENDELEA |
KIKISHIKA KASI KILIO |
afisa uhamiaji mkoa wa Tanga bwana Sixtus Nyaki amewataja watanzania hao kuwa ni Alhaj Miraj Shimbo na Halfan Mwaveso ambao walikuwa na wahamiaji wawili raia wa Ethiopia waliokamatwa wilayani Muheza baada ya kuingia katika bandari bubu zilizopo jirani na eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Kwa upande wa watuhumiwa walipohojiwa mara baada ya kutiwa mbaroni na askari wa uhamiaji mmoja wapo aliyefahamika kwa jina la Mwaveso aliyekuwa anaangua kilio wakati akihojiwa na mwandishi wa blog hii,amesema kuwa hausiki kabisa na biashara hii na amemsukumia lawama bosi wake kuwa ndiye aliyekuwa anawasafirisha baada ya yeye kuombwa akawakatie tiketi ya basi wahabeshi hao hali ya kuwa yeye hawafahamu.
Inadaiwa wasafirishaji wa wahamiaji haramu hupata kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wahamiaji hao ili waweze kuwasafirisha na mara nyingi wamekuwa wakiwasafirisha kwa njia ya malori hali ambayo imeshasababisha vifo vya wahamiaji haramu wengi sana kutokana na kukosa hewa na wengine wengi kukamatwa.
No comments:
Post a Comment