Saturday, August 31, 2013

UZINDUZI WA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TANZANIA THDR


NAIBU SPIKA  WA BUNGE JOB NDUGAI AKIFUNGA SEMINA YA  UZINDUZI WA MCHAKATOWA RIPOTI YA MAENDELEA YA BINADAMU TANZANIA  THDR UZINDUZI HUO ULIANDALIWA NA TAASISI YA UTAFITI YA MASAUALA YA KIUCHUMI NA KIJAMII ESRF ULIFANYIKA KWENYE MJINI DODOMA LEO KUTOKA KULIA  MKURUGENZI WA UNDP TANZANIA PHLIPPE POINST WA PILI KULIA NI WAZIRI WA FEDHA DR WILLIAM MGIMWA,WSA KWANZA KUSHOTO NI MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA UTAFITI WA MASUALA YA KIUCHUMI NA KIJAMII ESRF DR HOSEANA LUNOGELA NA WAZIRI WA ULINZI  SHAMSI VUAI


BAADHI YA WAJUMBE WA TAASISI YA UTAFITI YA MASUALA YAKIUCHUMI NA KIJAMII YA ESRF WALIOHUDHURIA UZINDUZI WA MCHAKATO WA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TAMZAMIA THDR ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PIUS MSEKWA MJINI DODOMA LEO

PICHA YA PAMOJA YA WABUNGE PAMOJA NA VIONGOZI WA TAASISI YA UTAFITI YA MASUALA YA KIUCHUMI NA KIJAAM  MARA BAADA YA UZINDUZI WA MCHAKATOWA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TANZANIA ILIYOFANYIKA MJINI DODOMA


WAZIRI WA ULINZI  SHAMSI NAHODHA VUAI AKIZINDUA MCHAKATO WA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TANZANIA  ULIANDALIWA NA TAASISI YA UTAFITI YA MASUALA YA KIUCHUMI NA KIJAMII ESRF ULIOFANYIKA MJINI DODOMA

BAADHI YA WAJUMBE WA TAASISI YA UTAFITI YA MASUALA YAKIUCHUMI NA KIJAMII YA ESRF WALIOHUDHURIA UZINDUZI WA MCHAKATO WA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TAMZAMIA THDR ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PIUS MSEKWA MJINI DODOMA LEO KUSHOTO NI KATIBU MKUU WA WIZRAYA FEDHA DKT SERVACIUS LIKWELILE

BAADHI YA WAJUMBE WA TAASISI YA UTAFITI YA MASUALA YAKIUCHUMI NA KIJAMII YA ESRF WALIOHUDHURIA UZINDUZI WA MCHAKATO WA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TAMZAMIA THDR ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PIUS MSEKWA MJINI DODOMA LEO

Friday, August 30, 2013

ETO'O AKUBALI PAUNI MILIONI 10 NA KUJIUNGA TENA DARAJANI KWA MORINHO


Parading: Eto'o has signed for Chelsea
Parading: Eto'o has signed for Chelsea
Pen to paper: Eto'o signs the contract in the presence of Chelsea club secretary and director David Barnard
SAMWEL ETO'O AKISAINI MKATABA MBELE YA KATIBU WA TIMU YA CHELSEA DAVID BARNARD
Pleased to be here: Eto'o has signed on a free transfer
ETO'O AKIONYESHA JEZI YA DARAJANI

Eto'o in a Chelsea shirt (as imagined by Sportsmail)
Full steam ahead: Samuel Eto'o arrived at St Pancras station on Wednesday night ahead of his move to Chelsea
Chelsea bound: Cameroon striker Eto'o arrives at St Pancras
Eto'o with Pini Zahavi
ETO'O AKIPEANA MKONO NA PINI ZAHAVI NA KULIA ANAONEKANA AKIELEKEA KWENYE GARI YAKE

Whisked away: Eto'o leaves St Pancras after arriving in London
Whisked away: Eto'o leaves St Pancras after arriving in London
                                                                          ETO'O AKIWA KWENYE GARI YAKE
Solution? Samuel Eto'o will seal his move to Chelsea as Jose Mourinho ends his striker search

Top target: Mourinho didn't select any strikers at Old Trafford and is known to be chasing Wayne Rooney
NDOTO ZA MORINHO ZILIANZA KWA ROONEY LAKINI NDOTO HIZO SASA ZIMEKUFA
Treble
ETO'O NA MORINHO WAKISHEREHEKEA FURAHA YA USHINDI WAKTI WAPO NA TIMU YA INTER MILLAN

PICHA MBALI MBALI ZIKIMUONESHA DIAMOND AKIMZAWADIA MZEE GURUMO GARI

AKIMKABIDHI GARI AINA YA TOYOTA FUNGARCO

MZEE GURUMO NDANI YA MKOKO WAKE

AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKABIDHI GARI MZEE GURUMO

GARI AINA YA FUNCARCO AMBAYO DIAMOND AMEMKABIDHI MZEE GURUMO


Mwanamuziki wa kizazi kipya anae kick kila kona Diamond Platnumz jana aliweka rekodi na kumbukumbu katika maisha yake pale alipomzawadia gari  Maalim Gurumo.

Diamond alimkabidhi mzee Gurumo gari hilo katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya number 1 katika ukumbi wa hoteli ya kimataifa Serena jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kumkabidhi gari hilo Diamond alisema alijiskia vibaya pale alipomsikia mzee Gurumo wakati akihojiwa redioni kuwa katika maisha yake ya muziki kwa miaka 53 hadi anastaafu,hajawahi kununua hata baiskeli.


MWANAJESHI WA TANZANIA AUAWA NA M23 DRC


PICHA YA ASKARI WA TANZANIA WAKIWA KATIKA SHUGHULI ZA UOKOAJI
ASKARI WA TANZANIA WANAOLIOPO KATIKA VIKOSI VYA KULINDA AMANI VYA UMOJA WA MATAIFA DRC
Askari wa Umoja wa Mataifa raia wa Tanzania ameuawa na wengine watano raia wa Afrika Kusini na Tanzania kujeruhiwa katika mapigano na waasi wa M23 huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Msemaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo Madnodje Mounoubai amesema askari huyo wa kulinda amani ameuawa katika mapigano yaliyojiri Jumatano wakati waasi walipokuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali ya Kongo Kinshasa wanaopata himaya ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Mapigano hayo yalijiri karibu na mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema askari huyo aliuawa baada ya kuangukiwa na maroketi ya waasi wa M23. Jana ngome za waasi wa M23 zilishambuliwa kwa helikopta za jeshi la Umoja wa Mataifa na mizinga ya jeshi la Kongo karibu na mji wa Goma. 

Jeshi la Kongo linapata msaada wa kikosi cha askari 3,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanaidhini maalumu ya kupigana ana kwa ana na makundi ya waasi wenye silaha katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini. Kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi wa Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWSSS!!!!!!!!!!!

RAMANI IKIONYESHA MAHALI ILIYOPO HABIB BANK KARIAKOO
WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI BAADHI YAO WAKIWA WAMEVALIA SARE ZA JESHI LA POLISI WAMEVAMIA HABIB AFRICAN BANK ILIYOPO KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM NA KISHA KUPORA NA KUTOWEKA NA MAMILIONI YA FEDHA ASUBUHI YA LEO

ULINZI MKALI KESI YA SHEIKHE PONDA ISSA PONDA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOROGORO.


Katibu    wa jumuiya na taasisi ya kiislamu nchini Shekh Ponda Issa Pondakatikati aliyekaa ,akiwazungumza na wakiri wake Juma Nasoro kabla  ya kusomewa mashtaka yake katika Mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa morogoro
...
 Askari wa Jeshi la Magerza kutoka Jijini Dar es Salaam wakimuongoza kuelekea Mahakama ya hakimu mkazi wa Morogoro Katibu    wa jumuiya na taasisi ya kiislamu nchini Shekh Ponda Issa Ponda kwajili kusikiliza kesiJijini Dar es Salaam wakimuongoza kuelekea Mahakama ya hakimu mkazi wa Morogoro Katibu    wa jumuiya na taasisi ya kiislamu nchini Shekh Ponda Issa Ponda kwajili kusikiliza kesi yake

TPSF:SERIKALI ISITISHE UGAWAJI WA VITALU VYA GESI

 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. (Picha na Francis Dande) 
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera ya uwekezaji nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte. 

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa kikao cha kwanza tangu bodi hiyo iteuliwe. Kushoto ni mjumbe wa Bodi hiyo, Arnold Kileo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imetakiwa kusitisha mara moja mpango wake wa ugawaji wa leseni za vitalu vya gesi hadi hapo itakapopatikana sera ya gesi ili kuwapa fursa watanzania kumiliki vitalu hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi, alisema kuwa endapo ugawaji wa vitalu hivyo utafanyika Oktoba mwaka huu kama ilivyopangwa, watanzania hawatakuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali hiyo.

Dk. Mengi ambaye alikuwa akizungumzia maazimio ya bodi hiyo iliyokutana mara ya kwanza jana tangu ilipoteuliwa hivi karibuni, alisema wakati Serikali iko mbioni kufanya mnada wa vitalu hivyo saba vya gesi, hakuna kipengere kinachomwezesha mtanzania kumiliki gesi hiyo.

Akizungumzia sera za uwekezaji kwa ujumla, Dk. Mengi alisema taasisi hiyo inaitaka Serikali kuingiza kwenye Katiba mpya inayokuja kipengere kinachowapa haki watanzania kuwa na ubia na wawekezaji wa nje badala ya kuwaachia wageni hao kumiliki rasilimali za hapa nchini kwa asilimia 100.

Alisema hali hiyo itawawezesha watanzania kuwa na hali ya kumiliki na kulinda rasilimali zao ambazo kwa sasa zinawanufaisha zaidi wageni kuliko watanzania wenyewe.

“Sisi tunaitaka Serikali ihakikishe kuwa shughuli yoyote ya uwekezaji wa kiuchimi, iwe na mtanzania ndani yake na watanzania hawa, wasishindwanishwe na wawekezaji wakubwa wan je,” alisema Dk. Mengi.

Naye Makamu mwenyekiti Salum Shamte, alisema kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha sheria ya manunuzi za umma inawanufaisha zaidi watanzania kuliko wawekezaji.

Alisema hivi sasa kiasi kikubwa cha fedha za Bajeti ya kila mwaka, zinatumika katika kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma na kazi hiyo imekuwa ikifanywa na wawekezaji badala ya kuwawezesha watanzania.

Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Dk. Mengi alisema kuwa asilimia 80 ya Bajeti ya mwaka huu wa fedha, itatumika kwa ajili ya manunuzi ya umma hivyo ni vyema kazi hiyo ikafanywa na watanzania.

“Ukiangalia bajeti ya mwaka huu, karibu asilimia 80, sawa na sh trilioni 14 zitatumika kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma za umma. Fedha hizi zikiingia kwa watanzania, zitachangia sana kukuza uchumi wa taifa,” alisema Dk. Mengi.

Wednesday, August 28, 2013

WATOTO WALIOUNGANA VIUNONI KUTENGANISHWA NA MADAKTARI 7 BINGWA MUHIMBILI

UPASUAJI wa kutenganisha watoto wawili waliozaliwa wameungana viunoni, unatarajiwa kufanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Katika upasuaji huo ambao mara ya mwisho ulifanyika 1980 chini ya Profesa Shija, madaktari bingwa saba wanatarajiwa kutenganisha watoto hao waliozaliwa Zanzibar. 
Katika upasuaji huo wa 1980, watoto waliotenganishwa walizaliwa wakiwa wameungana tumboni. Hata hivyo, haikuelezwa zaidi kama walipona au la.
Mmoja wa madaktari hao, Dk Zaituni Bohari, akizungumza na gazeti hili jana, alisema hadi kesho wakati wa upasuaji huo watoto hao watakuwa wamefikisha umri wa siku 23.
 
Dk Bohari alisema watoto hao, wamepungukiwa na viungo ambapo mmoja amepungukiwa zaidi-lakini hakutaka kuvitaja-kuliko mwingine ambaye hana sehemu ya haja kubwa.
 
Alisema hospitali hiyo ilipokea watoto hao wakiwa na siku nne kutoka visiwani humo na madaktari hao wamejiandaa kushiriki upasuaji huo kwa umakini mkubwa. Akifafanua, daktari huyo alisema hajui upasuaji huo utachukua muda gani kwa sababu unahusu masuala mengi ya kuzingatia na unahitaji utulivu wa akili.
Hofu ya mmoja Alieleza wasiwasi wake kuhusu uwekezano wa mtoto aliyepungukiwa viungo vingi kupona na kufafanua, kwamba ikibidi watajitahidi kuokoa mmoja ambaye anaonesha matumaini ya kuishi.
 
“Katika upasuaji huo, tutajitahidi mmoja apone na lengo likiwa ni kuokoa mwenye viungo vilivyokamilika na kumfanyia upasuaji mwingine wa kumtengenezea sehemu ya muda ya kutolea haja kubwa.
 
“Kwa sasa anatumia sehemu ya uke kujisaidia, jambo linaloweza kumsababishia magonjwa ya maambukizi kutokana na kupitisha uchafu huo mahali pasipotakiwa,” alisema Dk Bohari na kusisitiza kuwa madaktari bingwa wanaoaminika, watashirikiana kufanya upasuaji huo kwa karibu ili kuokoa maisha.
 
Akieleza historia ya watoto hao, Dk Bohari alisema walizaliwa Agosti 7 lakini hakutaja majina ya wazazi wao.

"WABUNGE WENGI WAMO KATIKA ORODHA YA DAWA ZA KULEVYA"-LUKUVI

MH WILLIAM LUKUVI

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.

Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.

“Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.

“Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu,” alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.

Katika swali lake ambalo lilisababisha kelele za kuzomea, Natse alitaka majina hayo yatajwe hadharani. Hata hivyo, hali ilitulia baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati na kusema: “Hii tabia ya zomeazomea siitaki humu ndani, acheni tabia hiyo lazima mumsikilize mtu kwa kile anachokisema kwanza lakini mtindo huu si mzuri...”

ASKARI WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WAJERUHIWA KONGO

Msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini MONUSCO ametangaza kuwa, kwa akali askari watatu wa vikosi hivyo akiwemo mwanajeshi mmoja wa Afrika Kusini, wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la kuvizia lililofanywa na waasi huko mashariki mwa nchi hiyo. Shambulio hilo lilitokea baada ya waasi wa M23 kurusha kombora katika eneo viliko vikosi vya UN umbali wa karibu kilometa nne kaskazini mwa mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini. 

Kwa mujibu wa msemaji wa MONUSCO, askari wengine wawili waliojeruhiwa ni Watanzania. Habari zaidi zinasema kuwa, kwa akali askari wa Afrika Kusini, wameshapambana mara mbili na waasi hao. 

Wakati huo huo, viongozi wa Pretoria, wamekanusha kujiri mashambulizi ya askari wa nchi hiyo dhidi ya waasi wa M23 nchini Congo DRC.

IRAN INATENGENEZA NDEGE YA KISASA YA KIVITA

Ndege ya kivita ya Qaher-313 iliyotengenezwa Iran na kuzindiliwa Tehran Februari 2 2013

Iran hivi sasa inatengeneza ndege ya kisasa kabisa ya kivita ambayo ni kati ya zana za kijeshi zilizotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini.
 
Hayo yamedokezwa leo na Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh, kamanda wa ngazi za juu katika Jeshi la Angani la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIAF).

Amesema utengenezaji wa ndege hiyo utaifanya Iran iache kabisa kutegemea ndege za kivita za kigeni hasa zile ambazo zinatumika kwa ajili ya mafunzo. Ameongeza kuwa Jeshi la Iran limechukua pia hatua za kujitengeneza makombora ya vita vya angani.

Katika miaka ya hivi karibuni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta yake ya ulinzi ambapo imeweza kujitosheleza katika uzalishaji wa zana na mifumo muhimu ya ulinzi. Februari pili mwaka huu, Iran ilizindua ndege yake mpya kabisa ya kivita ijulikanayo kama Qaher-313 yaani mshindi. Ndege hiyo yenye uwezo wa kukwepa rada ilibuniwa na kutengenezwa kikamilifu na wataalamu wa Iran. Ndege ya kwanza ya kivita kutengenezwa Iran ni ile ijulikanayo kama Azarakhsh. Aidha Iran imetengeneza ndege ya kivita ijulikanayo kwa jina la Saeqeh ambapo squadron yake ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2010.

Mara kwa mara Iran imeyahakikishia mataifa mengine kuwa uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu zimejengeka katika msingi wa kujihami.

WASIWASI WA UN KUHUSU MACHAFUKO CONGO

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na  kuongezeka machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
 
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, umoja huo una wasiwasi kuhusiana na kuongezeka mapigano baina ya jeshi la Congo DRC na wapigani wa waasi wa M23 huko mashariki mwa nchi hiyo. Farhan Haq amebainisha kwamba, usalama umevurugika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano baina ya jeshi la nchi hiyo na waasi wa M23. Aidha amesema, Umoja wa Mataifa umeanzisha uchunguzi kuhusiana na kuuawa waandamanaji wawili mjini Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, maandamano ambayo yalifanyika kulaani mauaji dhidi ya raia pamoja na ukosefu wa amani mashariki mwa nchi hiyo.

LEO KATIKA HISTORIA,KUTANA NA ,ARTIN LUTHER KING


Leo ni Jumatano tarehe 28 Agosti 2013.
Miaka 52 iliyopita katika siku kama ya leo, mwafaka na tarehe 28 Agosti 1963 Martin Luther King mwanaharakati mkubwa wa kutetea haki za Wamarekani weusi nchini Marekani, alihutubia umati mkubwa wa watu waliofanya mgomo wa kutaka wapewe haki ya kijamii nchini humo. Luther King ambaye ni Mmarekani mweusi alihutubia umati huo kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Lincoln mjini Washington. Kwenye mkutano huo, Martin Luther King alieleza ndoto yake ya kuwa huru Wamarekani weusi.
Siku kama ya leo miaka 264 iliyopita sawa na tarehe 28 Agosti 1749 alizaliwa Johann Wolfgang Von Goethe malenga na mwandishi mkubwa wa Kijerumani. Von Goethe alisoma na kujifunza mambo mbalimbali kama uchoraji na kadhalika katika mji aliozaliwa wa Frankfurt nchini Ujerumani, huku akiendelea na masomo yake ya taaluma ya sheria. Von Goethe ambaye anahesabiwa kuwa mmoja kati ya waenezaji wa fasihi ya lugha ya Kifarsi, alivutiwa mno na fasihi ya Kifarsi na hasa mashairi ya Hafidh, malenga na mshairi mashuhuri wa Kiirani. Mwandishi huyo wa Kijerumani alikipenda sana Kitabu Kitakatifu cha Qurani pamoja na dini ya Kiislamu. Johann Wolfgang Von Goethe alifariki dunia mwaka 1832.
Na siku kama ya leo miaka 617 iliyopita mtaalamu wa lugha na mwandishi mashuhuri wa zama hizo Majduddin Abu Tahir Muhammad Yaaqub Firuzabadi aliaga dunia.  Firuzabadi alikuwa pia hodari katika taaluma za hadithi na tafsiri ya Qur'ani na ameandika vitabu kadhaa katika taaluma hizo.
Hata hivyo kitabu mashuhuri zaidi cha mwanazuoni huyo ni "al Qamus" ambacho ni miongoni mwa kamusi muhimu za lugha ya Kiarabu. Vitabu vingine mashuhuri vya mwanazuoni huyo wa Kiislamu ni "Sifrul Saada" na "Tanwirul Miqyas".

Tuesday, August 27, 2013

PICHA ZINGINE TATU ZIKIONYESHA JINSI PUB YA SAMAKI SAMAKI MBEZI ILIVYOKUWA INATEKETEA KWA MOTO

Pub ya samaki samaki ilivyokuwa inateketea kwa moto

HALI HALISI YA MOTO

MAGARI YAKIPITA HUKU MOTO MKUBWA UKITEKETEZA

MTOTO WA MIEZI MIWILI AIBWA JIJINI DAR ES SALAAM

 
SHAMSA AKIELEZEA WALIVYOMUIBA MWANAE


Add caption

SHAMSA AMIRI MAMA MZAZI WA MTOTO RAHMA ALLY ALIYEIBIWA

SHAMSA NA PICHA YA MWANAE

SHAMSA AMIRI AKIONYESHA PICHA YA MTOTO WAKE

MTOTO RAHMA ALLY ALIYEIBIWA


SHAMSA AMIRI AKIELEZEAQ JINSI MTOTO WAKE ALIVYOIBIWA

MKAZI WA BUGURUNI GHANA SHAMSA AMIRI (27) AMEIBIWA MTOTO WAKE MWENYE MIEZI MIWILI YAPATA MWEZI MMOJA SASA ENEO LA BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM.

AKIELEZEAS MAZINGIRA YA KUIBIWA MTOTO HUYO,SHAMSA ANASEMA SIKU YA TUKIO ALIMPELEKA MWANAE HUYO RAHMA ALLY KATIKA CLINIC YA PLAN ILIYOPO BUGURUNI KWA MNYAMANI,WAKATI YUPO HOSPITALINI HAPO ALIMUONA DADA MMOJA AMBAYE ALIMCHANGAMKIA SANA,NA ALIVYOMALIZA KUMPIMA MTOTO WAKTI ANAONDOKA DADA HUYO NAE AKATOKA WAKAENDA PANDA NAE DALA DALA.

WAKATI WAPO KWENYE DALA DALA ANADAI ALIPEWA SODA NA HUYO DADA ALIVYOINYWA ANASEMA AKAWA ANAJISKIA KUCHOKA NDIPO HUYO DADA AKAMUOMBA AMSHIKIE MTOTO NA ANASEMA HAKUPINGA KWANI KILA ALICHOAMBIWA NA YULE DADA ALIKIFUATA KWA KUWA ALIKUWA HAJISIKII VIZURI NA ALICHOKA SANA,WALIVYOFIKA BUGURUNI AKAENDA NAE KUNUNUA NDIZI ZA KUPIKA,ALIVYOINAMA KUCHAGUA NDIZI YULE DADA AKATOWEKA NA MTOTO NA MPAKA SASA LICHA YA KUTAFUTA HUKU NA KULE HAKUNA MAFANIKIO YEYOTE. 

SHAMSA ANASEMA WAKATI MTOTO WAKE ANAIBIWA ALIKUWA NA MWEZI MMOJA NA SIKU 18,NA SIKU YA LEO MTOTO ANATIMIZA MIEZI MIWILI.

ANAOMBA YEYOTE ATAKAEMUONA MTOTO AMBAE PICHA YAKE IPO HAPO JUU ARIPOTI KITUO CHOCHOTE CHA POLISI AU APIGE SIMU NAMBARI 0656 757690.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...